SERIKALI IMERIDHIA KUPUNGUZA MIGOGORO YA MATUMIZI YA ARDHI NCHINI KWA KUTOA BAADHI YA MAENEO YA HIFADHI KWA WANANCHI

“Tunamshukuru Raisi wa awamu ya tano, Mheshimiwa J.P.Magufuli, amekuwa ni msumari wa majibu ambayo yataweka wanyama pori wetu maeneo salama zaidi na misitu yetu itasimamiwa kwa mustakabali wa sheria zisizoingiliana” alisema Zakaria Faustin baada ya kusoma taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu tarehe 23 Septemba 2019 kuelezea kufutwa kwa mapori tengefu 12 na hifadhi saba (7).

"Serikali ya Tanzania imeridhia kufuta Mapori tengefu 12  yenye ukubwa wa ekari 707.659.94 ambayo yamepoteza sifa ya kuwa hifadhi na yaweze kugawiwa kwa wananchi” alisema Waziri mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa.  Maamuzi haya yalitolewa baada ya Mawaziri wa kisekta waliochangia na kuandaa taarifa ya mapendelezo ya utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi nchini. Kwa kufuta mapori tengefu 12 ni hatua kubwa kwa Serikali kwani wawekezaji wengi wamechukua mashamba makubwa bila kuyaendeleza na wananchi kuachiwa na eneo dogo lisilokidhi mahitaji yao. Eneo hili linahitaji kutazamwa vyema kwani changamoto imekuwa maeneo yanafutiwa umiliki na hayarudi kwa wananchi hivyo kupelekea kuongezeka kwa migogoro ya ardhi, alisema bwana Masalu Luhula Mratibu wa kitengo cha ardhi na uwekezaji Jumuiko la Maliasilia Tanzania (TNRF).

Migogoro ya matumizi ya ardhi imekuwa ni changamoto nchini. Wananchi wengi wamekuwa wakilalamika juu ya kunyang’anywa Ardhi kwa ajili ya uhifadhi na uwekezaji. Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF) kwa kushirikiana na wanachama wake  limekuwa likifanya kazi kubwa katika kutatua migogoro ya ardhi na kushauri Serikali juu ya sheria kinzani zinazopelekea kuwa na migogoro juu ya matumizi ya ardhi na Maliasili kwa ujumla.

via ytCropper

 

Relevance: 
AttachmentSize
PDF icon Press release165.42 KB
Undefined