MKUTANO WA WADAU KUJADILIANA KUHUSU MABORESHO YA SHERIA YA WANYAMAPORI TAREHE 3 DESEMBA 2018

Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF) kwa kushirikiana na baadhi ya wadau wengine wa maliasili na utalii watakutana siku ya tarehe 3 Desemba 2018, kwenye mkutano wa siku moja kujadiliana juu ya utekelezaji wa Sheria ya uhifadhi wa wanyamapori na changamoto wadau wanazokumbana nazo katika utekelezaji wa sheria hiyo.

Matarajio:

  1. Wadau kuainisha vipengele vya sheria ya Wanyamapori ambavyo vinahitaji maboresho ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wake.
  2. Kuja na mapendekezo yatakayoboresho sheria ya wanyamapori
  3. Mpango wa utekelezaji wa muda mfupi kulingana na vipaumbele vya wadau.

Moja ya malengo ya mradi huu ni pamoja na kuelimisha Umma kuhusu sheria za uhifadhi, utekelezaji wake na kupata mapendekezo yatakayosaidia uboreshaji wa sheria hitoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo watunga sera, sheri na kanuni, wasimamizi na watekelezaji wa sheria hizo.

Wadau wanaoshiriki mkutano huu ni pamoja na Mazingira Network, Tanzania Association of Tour Operator, Tourism Confederation of Tanzania, Community Wildlife Management Area Consortium, The Nature Conservancy, Ujamaa Community Resource Team, Tanzania Private Sector Foundation, Maliasili initiative na Honey-guide foundation.

 

 

 

 

 

Relevance: 
Undefined